Kiungo mpya wa Simba Haruna Niyonzima amesema haikuwa rahisi
kwake kuhama kutoka Yanga kwenda Simba lakini kwa kuwa yeye ni mchezaji
na hajui ataishia wapi, alichukua uamuzi wa kuondoka Yanga pale wakati
ulipofika.
“Haikuwa rahisi kuhama Yanga lakini naamini kuna wana Yanga na
wapenzi wa Haruna wameumia lakini mimi niseme yote ni maisha, mimi
mcheza mpira siwezi kujua nitaishia wapi lakini kikubwa ni kufanya kazi
yangu. Nawashukuru Yanga, kwa sababu ni timu ambayo nimecheza misimu
mingi sana kuliko timu zote duniani,” Haruna Niyonzima.
Niyonzima ametambulishwa mbele ya mashabiki wa Simba siku ya Simba Day ambayo huadhimishwa na wana Simba August 8 kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment