Tume ya IEBC imesema kuwa hakuna udukuzi wowote uliofanyiwa mfumo wake wa kutoa matokeo ya uchaguzi kielektroniki.
Afisa mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema kuwa mfumo huo uko salama.
Akivihutubia
vyombo vya habari katika makao makuu ya IEBC katika eneo la Bomas
jijini Nairobi, amesema kwamba mfumo huo haukuingiliwa kabla, wakati na
hata baada ya uchaguzi.
Amesema kuwa madai ya upinzani kwamba
mfumo huo ulidukuliwa ili kumsaidia rais Uhuru Kenyatta kupata ushindi
hayana msingi wowote.
Amesema kuwa maafisa wa tume hiyo waliufanyia uchunguzi mfumo huo hususan funguo zake na wakati kwamba hakuna tatizo lolote.
''Hakuna
mtu aliyepewa funguo za kuingia katika mfumo huo hadi siku moja labla
ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa kuna maadili',alisema Chiloba.
Hatahivyo amesema kuwa tume hiyo imeweka ulinzi mkali dhidi ya wadukuzi.
''Iwapo una ripoti zozote kuhusu vitisho vya mfumo wetu
tushirikiane kwa sababu mfumo huu sio wetu bali ni wa raia wa
Kenya'',aliongezea.
Bw Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake
Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, amesema
wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC
Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya
IEBC.
Waziri huyo mkuu wa zamani amesema baada ya kuingia,
wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na
kupunguza matokeo yake.
Amesema anaamini hilo lilifanyika katika kaunti zote na kwamba wagombea wa NASA katika nyadhifa nyingine waliathirika pia.
IGAD tayari imesema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa njia ilio huru na haki
0 comments:
Post a Comment