Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa ameanza kuiva bana katika uzungumzaji wa lugha ya Kiswahili.
Chirwa anaweza kufanya mawasiliano na wachezaji wenzake kwa Kiswahili japo anaongea kama mtu mwenye kigugumizi katika utamkaji wa maneno lakini anaonekana kuanza kukifahamu vizuri.
Kuna muda staa huyo wa Yanga huwa anachanganya maneno pale anaposhindwa kutumia neno fasaha la Kiswahili.
Mzambia huyo amedai kuwa karibu na wachezaji wenzake, kumemfanya kukifahamu Kiswahili kwa haraka.
"Muda mwingi huwa nasikia Kiswahili kikizungumuzwa na wachezaji wenzangu huwa najifunza, sio kwamba hii ni lugha ni ngumu hapana,"alisema Chirwa.
0 comments:
Post a Comment