Jose Maourinho anasema kuwa matumaini ya Manchester United kumsaini mchezaji wa Real Madrid mzaliwa a wa Wales Gareth Bale hayapo tena.
Awali Mourinho alisema kuwa angepigania kuweza kumsaini Bale ikiwa Real Madrid ingetaka kumuuza.
"Nafikiri kila mtu anajua kuwa anataka kusalia," Mourinho alisema.
Rais wa Real Madrid Florentino Perez alinukuliwa na gazeti la Uhispania, Marca akisema kwa mabingwa hao wa Uhispania hawana mpango wa kumuuza Bale.
"Akili yangu iko katika kandanda na siwezi kuskiliza chochote." alisema Bale.
Bale 28, alijiunga na Real Madrid kwa kima cha pauni 85 akitokea Tottenham mwaka 2013.
Alitangaza kuwa na Madrid siku za usoni mwishoni mwa msimu akisema kuwa atakuwa na furaha kusalia na mabingwa hao wa Ulaya mara 12.
Madrid pia wanaripotiwa kuwa na mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Monaco Kylina Mbappe kwa pauni milioni 160.
0 comments:
Post a Comment