Dar es Salaam. Uwanja wa Taifa ulisimama kwa muda wakati wachezaji wawili wa Simba, Emanuel Okwi na Haruna Niyonzima wakutambulishwa.
Viongozi mbalimbali waliokuwemo jukwaa kuu pia hawakusita kupiga makofi wakati Niyonzima na Okwi wakitambulishwa.
Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba ambaye ni shabiki wa kugalagala wa Yanga alishindwa kuzuia hisia zake baada ya Niyonzima na Okwi kutambulishwaa.
Okwi na Niyonzima waliwahi kuichezea Yanga na msimu huu wamekuwa gumzo baada ya kununuliwa na Simba.
Wakati huo huo; Kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto ameridhia kumkabidhi jezi namba 8 kiungo mpya Niyonzima.
Niyonzima amesajiliwa kuitumikia Simba msimu hu baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga.
"Limetokea jambo kubwa kambini, Kazimoto ameridhia kumpa jezi Niyonzima," amesema Haji Manara kabla ya kuanza kuwatambulisha wachezaji wa timu hiyo
0 comments:
Post a Comment