HABARI kuwa kiungo wa Chelsea Nemanja Matic anatarajiwa kusajiliwa na Kocha Jose Mourinho ndani ya Manchester United kwa dau nono siyo jambo geni kwa kocha huyo raia wa Ureno.
Mourinho hajawahi kuwa na aibu katika suala la matumizi ya fedha za
kusajili kwake suala la kuwataka mabosi wake kumwaga fedha nyingi
kumpata mchezaji anayemtaka siyo kitu kigumu kwa kuwa amekuwa akifanya
hivyo kisha mtihani unabaki kwake kuhakikisha anatwaa mataji.
Tabia hiyo ameifanya kote alikopita iwe ni Porto, Chelsea, Inter, Real Madrid, Chelsea na sasa anaifanya akiwa ndani ya Mashetani Wekundu.
Inaelezwa kuwa Matic anaweza kusajiliwa kwa pauni milioni 35, dau ambalo linaonekana ni nono.
Kutokana na hali hiyo, tujikumbushe wachezaji wanaoweza kuunda
kikosi kwa kila nafasi waliosajiliwa kwa gharama kubwa na kocha huyo.
Kipa Asmir Begovic, Chelsea Pauni 8m (2015)
Alisajiliwa akitokea Stoke City, bahati nzuri k w a Mourinho katika
nafasi hii ni kuwa makipa wengi aliowakuta kwenye timu alizofundisha
walikuwa na uwezo mkubwa, h i v y o h a k u t u m i a gharama kubwa
kusajili mbadala.
Baadhi ya majembe aliyoyakuta ni Petr Cech, Iker Casillas na David De Gea.
Beki wa kulia Paulo Ferreira, Chelsea Pauni 13.2m (2004)
A l i k u w a mmoja wa mabeki hodari wa kocha huyo amb a y e a l i f
a n y a kazi nzuri alipokuwa Chelsea. Kwenye nafasi hii pia hajatumia
fedha nyingi kwa kuwa huyu alimsajili miaka 13 iliyopita.
Beki wa kati Eric Bailly, Manchester United Pauni 30m (2016)
Aliposajiliwa jina lake halikuwa maarufu sana, lakini kwa sasa watu
wote wa soka wa England na Ulaya wanamjua vizuri kutokana na kiwango
kizuri alichokionyesha ndani ya msimu mmoja.
Ilionekana kama dau alilosajiliwa ni kubwa kuliko jina lake lakini
ameweza kuishi ndani ya thamani aliyonayo, ndiye chaguo la kwanza la
kocha huyo hadi sasa, kilichomrudisha nyuma ni kuwa na majeraha tu.
Beki wa kati Victor Lindelof, Manchester United Pauni 31m (2017)
Beki mpya kutoka Benfica ambaye hajagusa hata nyasi za uwanjani akiwa kwenye jezi yake hiyo mpya.
Inaonekana Mourinho anajua anachokihitaji kutoka kwake, wengi hawana
ufahamu mkubwa juu yake lakini inavyoonekana anaweza kufiti japokuwa
hilo ni deni kubwa kwake.
Beki wa kushoto Fabio Coentrao, Real Madrid Pauni 26.5m (2011)
Baada ya kuonyesha uwezo mzuri akiwa ndani ya Benfica na katika
michuano ya Kombe la Dunia ya 2010, Coentrao alielekea Madrid kujiunga
na Mreno mwenzake. Bahati mbaya uwezo wake ukawa wa kawaida na hakupata
mafanikio makubwa kama ilivyotegemewa.
Kiungo wa kulia Willian, Chelsea Pauni 30m (2013)
Ni aina ya wachezaji ambao wanaonekana hawana vipaji vikubwa lakini
ni wepesi wa kujifunza na kujituma. Alikuwa mtumishi mwenye kuaminiwa
kwa kocha huyo ambaye alikuwa akimtumia katika mechi muhimu kwa kumpa
majukumu ya kukaba na kushambulia.
Kiungo wa kati Paul Pogba, Manchester United Pauni 89m (2016)
Ukitaja jina la Pogba unataja fedha. Mchezaji ghali zaidi duniani
ambaye usajili wake ulizua gumzo kutokana na kuonekana kama thamani yake
imekuzwa kupitiliza.
Alirejeshwa klabuni hapo baada ya kuondoka akiwa mdogo, akapewa
mzigo mkubwa wa kutakiwa kuishi kwenye thamani ya fedha aliyosajiliwa,
amekuwa na msimu mzuri japo kuna wakati alipata wakati mgumu uwanjani.
Kiungo wa kati Luka Modric, Real Madrid Pauni 33m (2012)
Kiungo fundi ambaye usajili wake ulizua gumzo kutokana na Spurs
kusita kumuuza, aliposajiliwa alionyesha ufundi kwenye kuuchezea mpira
na mpaka sasa bado ni tegemeo kwenye kikosi cha kwanza.
Kiungo wa pembeni Henrikh Mkhitaryan, Man United Pauni 26.3m (2016)
Alianza kwa kuwa na maisha magumu kutokana na kutozoea mazingira,
mara kadhaa alilaumiwa na kocha wake lakini baadaye alianza kuzoea
mazingira na kucheza soka zuri.
Mshambuliaji Diego Costa, Chelsea Pauni 35m (2014)
Mourinho amekuwa na kawaida ya kuwa na straika mmoja matata ambaye
ni tegemeo. Ndiyo ilivyokuwa kwa Costa, alimsajili licha ya kuonekana
alikuwa ni mchezaji mkorofi, lakini alipata mafanikio na kuwa staa wa
Chelsea.
Mshambuliaji Andriy Shevchenko, Chelsea Pauni 30m (2006)
Alisajiliwa kwa gharama kubwa licha ya kuwa hakuwa chaguo la
Mourinho, matokeo yake akawa na maisha magumu na mbinu za kocha huyo
hazikumsaidia kuamka na kurejesha enzi zake kama ilivyokuwa.
MANCHESTER, England
0 comments:
Post a Comment