Thursday 24 August 2017

TSHISHIMBI, HARUNA DILI DAR

HUKO mtaani, wauza jezi wanapiga pesa ndefu za mauzo ya jezi za kiungo mpya wa Yanga, Mkongo Kabamba Tshishimbi siku chache tu baada ya kutua nchini na kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.
Tshishimbi ni usajili mpya lakini katika soko la jezi, yeye ndio anaongoza kwa jezi hiyo namba 24 akipambana na Mnyarwanda Haruna Niyonzima aliyejiunga na Simba na kukabidhiwa jezi namba nane.
Mwanaspoti imeshuhudia uuzwaji wa jezi sehemu mbalimbali kama Kariakoo, Manzese na stendi ya mabasi yanayokwenda mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam.
Muuzaji wa jezi hizo nje ya stendi ya mabasi Ubungo, Issa alisema: “Biashara ya jezi ni nzuri kwa kipindi hiki cha maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga, na safari hii jezi inayouzika kwa wingi ni ya Tshishimbi anamzidi kidogo Niyonzima”
“Jezi hizi zina vipindi, mwanzoni kipindi cha usajili kilipoanza, Shiza Kichuya kwa Simba na Ibrahim Ajibu kwa Yanga walikuwa juu, kisha Niyonzima alipojiunga Simba akashika soko kwa kiasi na sasa Tshishimbi ni kama wanachuana.”
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive