Manchester United na Paris
St-Germain wako tayari kutoa £174m kumfungua mshambuliaji wa Barcelona
Neymar kutoka kwa mkataba wake katika klabu hiyo iwapo mchezaji huyo
ataamua kuihama klabu hiyo ya Uhispania (Don Balon kupitia Daily Star).
Arsenal
wanakaribia kutangaza usajili wa winga kutoka Algeria, Riyad Mahrez, 26
ambaye anaichezea Leicester City (Calciomercato).
Paris Saint Germain wamemuulizia kiungo wa Liverpool Philippe
Coutinho, 25, huku Liverpool wakisema mchezaji huyo kutoka Brazil ana
thamani ya pauni milioni 87 (Daily Mirror).
Chelsea wana matumaini
wataweza kufanikisha mpango wa kumsajili beki wa kushoto kutoka Brazil,
Alex Sandro, 26, huku mazungumzo na Juventus yakitarajiwa kufanyika
Jumatatu (Daily Telegraph).
Antonio Conte anakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City katika
kutaka kumsajili beki wa kati wa Roma Antonio Rudiger, 24. Barcelona
pia wanataka kumsajili Leonardo Bonucci, 30, ambaye Chelsea wanamtaka,
na Juventus wamempa mkataba mpya Sandro ili kumsawishi asiondoke (Daily
Mirror).
Jurgen Klopp ameiambia Liverpool kuongeza bidii katika
kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, ambaye atakuwa na
mazungumzo na klabu yake kuhusu mustakbali wake nchini Ujerumani
(Times).
Nahodha wa zamani wa England na Chelsea John Terry, 36,
anatazamiwa kuthibitishwa kuwa mchezaji wa Aston Villa siku ya Jumatatu
(Daily Telegraph).
Kocha mkuu wa Monaco Leonardo Jardim ana matumaini kuwa Kylian
Mbappe, 18, hataondoka, lakini amekiri kuwa wachezaji wengi huenda
wakaondoka msimu huu (RMC).
Tottenham wamepanda dau kwa mara ya pili la pauni milioni 27 kumtaka kiungo wa Sporting Lisbon Adrien Silva, 28, (A Bola).
Chelsea wamemuulizia beki wa Real Madrid Danilo, 25 (Marca).
Beki
wa Paris St-Germain anayenyatiwa na Manchester City, Marquinhos, 23,
amesaini mkataba mpya wa mude mrefu kubakia Ufaransa (Independent).
Newcastle wanafikiria kumchukua beki wa Arsenal Kieran Gibbs (Daily Mirror).
Paris Saint-Germain wamemuulizia kiungo mshambuliaji wa Liverpool
Philippe Coutinho, huku Barcelona pia wakimnyatia mchezaji jhuyo kutoka
Brazil (Daily Mirror).
0 comments:
Post a Comment