Monday, 3 July 2017

MTANZANIA ANAECHEZEA UJERUMANI ATUA NCHINI


MSHAMBULIAJI wa RB Leipzig inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, Yussuf Poulsen, raia Dernmark, mwenye asili ya Tanzania, yupo nchini tangu Alhamisi ya wiki iliyopita akila bata.

Poulsen ambaye alizaliwa nchini Denmark na baba yake ambaye ni marehemu aliyefariki kwa Ugonjwa wa Kansa, amekuwa na kawaida ya kutua nchini kuwasalimia ndugu zake ambao makazi yao yapo Tanga.

Babu wa staa huyo ambaye msimu uliopita alicheza mechi 25 za Bundesliga na kuisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Bayern Munich, Abdallah Hamza ‘Babu’, amesema Poulsen alitua nchini Alhamisi iliyopita akitokea Ujerumani na kuungana na dada zake Kigoli na Samira ambao wao walitokea Dernmark.

Jana Jumapili Poulsen alikwea pipa kwenda Arusha akiwa na Kigoli ambapo wamekwenda kutembelea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro na wanatarajiwa kuondoka muda wowote ndani ya wiki hii kwa kuwa anawahi kwenda kwenye maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa).

“Poulsen yupo hapa tangu Alhamisi, alitokea moja kwa moja Ujerumani, tunamshukuru kwa kuwa amekuwa akija kutusalimia kila anapopata muda, leo (jana) anakwenda Arusha huko atakaa kidogo, kisha ataondoka kurejea kazini kwake,” alisema Babu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive