Everton inatarajia kukamilisha malipo ya pauni milioni 25 ya kumsaini beki wa Uingereza Michael Keane hivi leo.
Keane, 24, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kwa saa 24 zilizosalia kabla ya kukamilisha uhamisho wake rasmi.
Everton itatangaza rasmi usajili kwa mshambuliaji chipukizi Sandro Ramirez kutoka mjini Malaga huko Uhispania.
Usajili wa Keane na usajili wa Sandro, utasababisha Everton kutumia zaidi ya pauni milioni 90, fedha ambazo wametumia katika kipindi cha sasa cha kuhama kwa wachezaji.
Everton tayari imemsajili mlinda lango wa England, wa kikosi cha chini ya miaka 21, Jordan Pickford kwa kitita cha pauni milioni 30 na kumnunua nahodha wa Ajax Davy Klaaassen kwa uhamisho wa pauni milioni 24.
Mshambuliaji wa Nigeria Henry Onyekuru aliwasili kutoka KAS Eupen mjini Ubelgiji kwa kitita cha pauni milioni 7 ingawa atasalia katika klabu hiyo ya Anderlecht kwa muda wa miezi 12.
Kuwasili kwa Keane haitakuwa mwisho wa Everton kutumia pesa nyingi chini ya meneja Koeman ambaye ana lengo la kuijaribu Swansea City iwapo watamuhifadhi kiungo wa kati mwenye miaka 27 kutoka Iceland Gylfi Sigurdsson.
The Toffees pia watafanya biashara na burnely katika msimu wa joto baada ya ripoti kwamba wameanza mazungumzo dhidi ya mshambuliaji Andre Gray
0 comments:
Post a Comment