Katika
hali ya kawaida si nadra kumkuta mzee wa miaka zaidi ya 70 akiwa na nguvu kiasi
hata cha kubeba ndoo moja tu ya maji , sasa leo nimeipata ya babu wa miaka
77 kutoka mji wa Akwa Ibom, Nigeria ambaye ana uwezo wa kuvuta gari kwa
kutumia shingo yake.
Babu huyo
amefahamika kwa jina la Sampson, ila yeye anataka afahamike kwa jina la
African Superman, ana uwezo pia wa kuweka mkono wake juu na wanaume 10
wakabembea bila kuushusha mkono wake chini. Pia ana uwezo wa kutafuna
chupa, kuvuta gari kwa kutumia meno, na hata wanaume 15 wenye nguvu wakijaribu kuvutana naye, hujikuta wakishindwa.
0 comments:
Post a Comment