Friday, 28 July 2017

ALIYEMPA MBWA JINA LA BUHARI AACHILIWA HURU NIGERIA



Mashtaka yameondolewa dhidi raia mmoja wa Nigeria aliyemuita mbwa wake Muhammadu Buhari.
Joachim Iroko mfanyibiashara wa sokoni ambaye anajulikana kama Joe Fortemose Chinakwe alikamatwa 2016 akishutumiwa kwa kufanya kitendo ambacho kinaweza kusababisha ghasia.

Jaji mmoja kusini Magharibi mwa jimbo la Ogun alibaini kwamba upande wa mashtaka ulifeli kutoa, Wakosoaji waliwashutumu maafisa wa polisi kwa kukiuka uhuru uliopo.

Wakati huohuo msemaji wa rais Garba Shehu alisema kwamba bwana Buhari amekuwa akicheka kuhusu habari hiyo na kusema kuwa mtu yeyote aliyekuwa akimhusisha na kisa hicho cha mbwa haelewi.

Akizungumza na gazeti la kila siku nchini Nigeria ''The vanguard'' baada ya uamuzi huo ,bwana Iroko alisema kuwa hakupatikana na hatia na kuwashukuru waliozungumza kwa niaba yake.
Wakili wa bwana Iroko alisema kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuwasilisha mashahidi na kwamba mlalamishi pia hakuwepo.

Mtu huyo aliyewasilisha malalamishi yake mnamo mwezi Agosti 2016 aliripotiwa kuwa jirani.
Bwan Iroko alitembea na mbwa wake huku jina Buhari likiwa limeandikwa katika pande zote mbili za mnyama huyo katika eneo ambalo rais Buhari ana wafuasi wengi ,polisi walisema.

Maafisa walisema kuwa walikuwa na waiswasi kwamba hatua hiyo huenda ingewachokoza watu, ijapokuwa alisistiza kuwa alifanya hivyo ili kumpongeza na kwamba watu hawakumuelewa.
Bwana Iroko alisema huwapatia majina mbwa wake baada ya watu mashuhuri walio na mfano bora , na kwamba wengine amewaita Nelson Mandela na Obama.

''Nilimtaja mbwa wangu Buhari , ambaye ni shujaa wangu....Upendo wangu kwa Buhari ulianza wakati alipokuwa mkuu wa jeshi'', Baadaye aliviambia vyombo ya habari kwamba amepokea vitisho kifo kufuatia hatua hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive