Friday, 28 July 2017

FRANCIS DAMIAN AITOA TANZANIA KIMASOMASO






Timu ya taifa ya Tanzania ya mchezo wa riadha ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 imerejea kwa kishindo leo baada ya  kutwaa medali ya shaba ya michuano ya sita ya dunia ya vijana ya Jumuia ya Madola (Bahamas 2017 Commonwealth Youth Games) yaliyomalizika hivi  karibuni huko nchini India.

Mwanariadha wa Tanzania, Francis Damian amefanikiwa kushika nafasi ya tatu  katika mashindano hayo na kupata medali ya shaba kwenye mbio hizo kwa upande wa wavulana baada ya kukimbia umbali wa mita 3000 akitumia muda wa 8.37.51 wakipishana kwa sekunde 13.55 na mshindi wa kwanza Mkenya na sekunde 2.36  kwa mshindi wa nafasi ya pili ambaye ni raia wa Canada.

Kwa kutwaa medali hiyo, Damasi Francis ameiwezesha Tanzania kushika nafasi 19 kwenye ushindi wa jumla wa riadha nakufungana na Botswana, Cyprus, pamoja na Afrika Kusini.

Na kufanikiwa kushika nafasi ya 31 kwa ushindi wa jumla wa michezo yote na kufungana na  Nchi za Grenada,Namibia na Rwanda.

Katibu mkuu wa wizara ya Habari , Utamaduni ,Sanaa na Michezo, Elisante Ole Gabriel ameongoza mapokezi ya viongozi na wachezaji hao waliowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius k . Nyerere hii leo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive