Friday 28 July 2017

VIKWAZO VYA IRAN,URUSI NA KOREA KUSINI VYAPITISHWA

US President Donald Trump and Russia's President Vladimir Putin shake hands during a meeting on the sidelines of the G20 Summit in Hamburg, Germany, on July 7, 2017.Haki miliki ya picha
Bunge la Senate nchini Marekani limepiga kura ya kuziwekea vikwazo vipya Urusi, Iran na Korea Kaskazini licha ya pingamizi kutoka Ikulu ya White House.
Bunge la waakilishi liliidhinisha mswaada huo mapema wiki hii kwa kura nyingi.
Baada ya mswaada huo kupita katika mabunge yote sasa utapelekwa kwa Rais Donald Trump kuwekwa sahihi.
Lakini bwana Trump anataka kuboresha uhusiano na Urusi na anaweza kuukataa licha na uungwaji mkono uliopata.
Vikwazo hivyo ni vya kuiadhibu Urusi zaidi kufuatia hatua za kulimega eneo la Crimea kutoka Ukrain mwaka 2014.
Lakini mjadala kuhusu vikwazo hivyo vipya unafanyika huku uchunguzi kuhusu hatua za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 ukiendelea.
Bwana Trump mara nyingi amekana kuwa Urusi iliingilia uchaguzi huo kusaidia kampeni yake.
Waandishi wa masuala ya siasa wanasema kuwa ikiwa Trump atajaribu kuukataa mswaada huo basi itakuwa ishara tosha kuwa anaiunga mkono sana Urusi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive