Friday, 28 July 2017

BILL GATES ACHUKUA TENA UONGOZI WA MTU TAJIRI DUNIANI

Bill Gates ampiku Bezos na kuwa mtu tajiri zaidi dunia
Boss Jeff Bezos alimpiku kwa muda mchache Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani siku ya Alhamisi kufuatia kupanda kwa hisa za mfanyibiashara huyo kabla ya ripoti ya mapato yake ,kabla ya hisa hizo kushuka tena.
Mfanyibiashara huyo ambaye alikuwa nambari nne duniani miongoni mwa watu matajiri zaidi duniani katika kipindi cha mwanzo wa mwaka alimpiku Bill Gates mapema siku ya Alhamisi baada ya hisa zake za kampuni ya Amazon kupanda asilimia 1.8 na kufikia dola 1,071.
Hatahivyo hisa hizo baadaye zilianguka na hivyobasi kufunga zikiwa zimeshuka kwa asilimia 0.7 kwa zikiwa dola 1,046, hatua inayoonyesha kwamba Bezos bado hajamshinda Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani katika orodha ya jarida la Forbes.
Bezos sasa ana thamani ya dola bilioni 88.5.
Bei hiyo ya hisa ilijiri saa chache kabla ya Amazon kutangaza mapato ya robo ya mwaka ambapo ilisema kuwa faida imeshuka kwa asilimia 77.
Hii inatokana na hatua yake ya kuimarisha uwekezaji katika video na upanuzi wa kimataifa.
Gates ambaye ana thamani ya dola bilioni 89.7 amekuwa mtu tajiri zaidi duniani tangu mwezi Mei 2013.
Bilionea huyo ametoa dola bilioni 31.1 ya mali yake kwa mashirika ya hisani.
Kwa upande wake Bezos ametoa ufadhili wa dola milioni 100 pekee kulingana na Forbes.
Bezos amekuwa nyuma ya Gates kwa wiki kadhaa, akiwa na thamani ya dola bilioni 89.3 kabla ya kupanda siku ya Alhamisi.
Jeff Bezos alimpiku Bill Gates mapema siku ya Alhamisi baada ya hisa zake za kampuni ya Amazon kupanda asilimia 1.8 na kufikia dola 1,071.
Mali yake imeongezeka kwa dola bilioni 24.4 mwaka 2017 huku Amazon ambayo inashilikia asilimia 17 ya hisa zikipanda kwa asilimi 40.
Bezos amempiku bilionea Amancio Ortega ambaye ana thamani ya dola bilioni 82.7 na Warren Buffet mwenye thamani ya bilioni 74.5.
Bilionea huyo wa teknolojia alianzisha kampuni ya Amazon 1994 kama duka la vitabu katika gereji yake mjini Seattle.
Amazon sasa ni mojawapo ya kampuni 50 kubwa duniani ikiwa na duka la mtandaoni na vipindi vya runinga.
Ufanisi wa Amazon Prime, umechangia pakubwa ukuwaji wa kampuni hiyo mwaka huu mbali na umaarufu wa Echo Speaker.
Bezos pia inamiliki gazeti la Washington post na kampuni ya safari za angani Blue Origin.
Pia inamiliki hisa katika kampuni pinzani ya Google, akiwa ndio mtu wa kwanza kuisadia kampuni hiyo ya utafutaji mbali na Airbnb na Uber.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive