WAKILI wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika, Tundu Lissu, Fatma Karume amefungua kesi ya madai Mahakama
Kuu ya Tanzania dhidi ya Inspekta wa Polisi Eugene Mwampondela wa Kituo
Kikuu cha Polisi Dar es salaam.
Katika kesi hiyo, Fatma anahitaji alipwe na Inspekta Mwampondela Sh
bilioni moja kwa kosa la kumwingilia mwilini mwake, kumbugudhi na
kumzuia kufanyakazi yake (assault, battery, misfeasance in public
office).
Fatma amesema Inspekta Mwampondela alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu hali iliyomsababishia maumivu kwenye mkono wake.
“Aliniambia kuwa ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha
mahakamani ili amweleze jaji ni nani aliyemtuma, na mimi sitaki kushikwa
shikwa mwili wangu kwa hiyo naomba anilipe shilingi bilioni moja ili
liwe fundisho kwa wengine,” amesema Fatma.
Fatma ambaye ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa Singida Mashariki
alikumbana na kadhia hiyo wakati akiwa katika harakati za kumtetea mteja
wake ili aweze kupata dhamana.
CHANZO: MTANZANIA
0 comments:
Post a Comment