NDOTO ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva
ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ilitimia juzi Jumatano
baada ya kiungo huyo kupaa hadi nchini Morocco kwa ajili ya kumalizana
na DifaĆ¢ Hassani El Jadidi kabla ya kujiunga nayo rasmi.
Msuva anaikacha Yanga aliyodumu nayo kwa miaka mitano tangu alipoh a
mia klabuni hapo akitokea Moro United mwaka 2012, baada y a kukamilika
kwa dili hilo ambalo limesimamiwa na meneja wake, Jonas Tiboroha. Ndani
ya klabu hiyo ya Difaa El Jadidi, Msuva ataungana na winga, Ramadhan
Singano ‘Messi’ ambaye alishatangulia kujiunga na kikosi hicho akitokea
Azam FC ambayo alimaliza mkataba.
Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa saba wa Kitanzania kwenda kucheza
soka la kulipwa nje ya nchi. Wengine ni Rashid Mandawa aliyepo
Botswana, Elias Maguri anayecheza Oman, Thomas Ulimwengu (Sweden),
Mbwana Samatta (Ubelgiji), Farid Mussa (Hispania) na Abdi Banda
aliyejiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini. M u d a mfupi kabla ya Msuva
kukwea pipa kuelekea Morocco juzi Jumatano, Championi Ijumaa, lilipata
nafasi ya kuzungumza naye na hapa anafunguka kama ifuatavyo:
NINI UTAKACHOKIKUMBUKA NDANI YA YANGA?
“Daaah! Kuna vitu vingi sana nitavimisi baada ya kuondoka Yanga,
siwezi kuvielezea sana lakini kikubwa ni juu ya utani ambao niliuzoea
kutoka kwa wachezaji wenzangu, lakini hata kuzurura kwani nilishazoea
nikitokea mazoezini naenda maskani ila huko Morocco sidhani kama
nitafanya hivyo. “Nikiwa huko nitawakumbuka sana washikaji zangu ambao
wamenifanya niwe hapa na wale ambao nimekaa na kushirikiana nao kwa
kipindi chote nikiwa Yanga.
UMEJIPANGAJE KUISHI NJE YA TANZANIA?
“Sehemu yoyote ile ukishazoea basi hakuna tatizo lolote lile,
najua nitakuwa mgeni kwa siku kadhaa zile za mwanzo lakini baada ya hapo
mambo yataenda vizuri. “Itakuwa siyo rahisi kwani huko kila kitu ni
kipya ila nitazoea na kuendana na maisha ya huko, kikubwa ni suala la
muda tu na kujichanganya na wenzangu.
VIPI KUHUSU LUGHA YAO, INAPANDA? “Sijajua maana nitakuta
wanazungumza lugha gani lakini ukija kwenye soka haitakuwa ngumu
kuwasiliana na wenzangu kwani mnapokuwa uwanjani mnaongea lugha moja tu
ya kimpira. “Shida itakuwa kwenye vitu vingine jinsi ya kuvipata ila
uwanjani sitapata sana taabu, lakini kadiri nitakavyokaa ndivyo nitazoea
tu sina hofu na hilo.
UNAIONAJE YANGA YA SASA?
“Iko vizuri, hakuna tofauti na timu am
bayo mimi naiacha na ile ya msimu uliopita kwani wachezaji wengi wamebaki na hata kwa wale waliondoka nafasi zao zimezibwa vizuri. “Ukinitoa mimi ninayeondoka naamini hawa waliobaki wataifanya kazi nzuri na kuendeleza mafanikio ambayo tumeyapata wakati ambao nilikuwepo.
bayo mimi naiacha na ile ya msimu uliopita kwani wachezaji wengi wamebaki na hata kwa wale waliondoka nafasi zao zimezibwa vizuri. “Ukinitoa mimi ninayeondoka naamini hawa waliobaki wataifanya kazi nzuri na kuendeleza mafanikio ambayo tumeyapata wakati ambao nilikuwepo.
UNAJISIKIAJE UNAVYOIACHA YANGA?
“Kiukweli natamani niendelee kuwepo lakini ndiyo hivyo hakuna namna,
umeshafika wakati sasa inabidi niondoke kwenda kucheza soka sehemu
nyingine tofauti na Yanga. “Najisikia vibaya kuachana na sehemu
niliyopata furaha, lakini hakuna namna inanibidi tu niondoke nikatafute
maisha sehemu nyingine.
NINI MIPANGO HUKO?
“Nimejipanga kucheza kwa muda mfupi na kwa juhudi kubwa ili nionekane
na timu nyingine, sitaki safari yangu iishie Morocco, namaani s h a k w
a m b a nitaondoka huko kama nilivyofanya hapa Yanga. “Hiyo ni njia tu
ya kwenda kucheza soka Ulaya, kama a m b a v y o n i m e k u w a
nikiwaza nifike alipo m s h a m b u l i a j i mwenzangu, Mbwana Samatta
ambaye kila mara amekuwa akinipa moyo wa kupambana. Unadhani itakuwa
rahisi kutamba Morocco? “Hakuna linaloshindana, naamini kama nikicheza
kwa juhudi kubwa na kufuata maelekezo ya kocha atakayonipa basi nina
nafasi kubwa ya kuendeleza kile ambacho nimekifanya kwa miaka mitano
niliyokaa hapa Yanga,” anasema Msuva.
0 comments:
Post a Comment