DAR ES SALAAM: Mapema leo
asubuhi, lori la maji taka limechafua hali ya hewa kwenye Barabara ya
Morogoro baada ya kumwaga ‘mzigo’ (maji yenye kinyesi) katikati ya
barabara hiyo maeneo ya Ubungo Mataa na kusababisha taharuki na harufu
kali.
Kwa mujibu wa mshuhuda wa tukio hilo,
inasemekana kuwa lori hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Rombo Kimara
ambapo baada ya kufika Ubungo kwenye mataa ya foleni, mfuniko wa tanki
uliftyatuka ndipo likaanza kumwaga uchafu huo barabarani.
Baada ya kuona hali hiyo, dereva wa lori hilo alitoka mbio na kwenda kuziba eneo ambapo uchafu huo ulikuwa ukitoka.
Hata hivyo watumiaji wa barabara hiyo na
wafanyabiashara wa eneo hilo hasa wamachinga wameshangazwa tukio hilo
huku wakieleza kuwa ilitakiwa dereva na kondakta wa gari hilo
wahakikishe mfuniko wa tanki umekaza kabla ya kuanza safari ili kuzuia
ajali kama hizo ambazo zinaweza kuepukika kwa kuzingatia umakini wa
kazi.
Aidha wananchi hao wameitaka Manispaa ya
Jiji la Dar es Salaam imchukulie hatua zinazostahili mmiliki wa gari
hilo na dereva wake ikiwa ni pamoja na kumtoza faini au kusafisha
barabara kutokana na adha aliyoisababisha ili liwe funzo kwa wamiliki na
madereva wengine wa magari ya maji taka.
0 comments:
Post a Comment