Gari lake lilivyopigwa risasi.
MBUNGE wa Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumpiga risasi zinazodaiwa kuwa tano.
Matundu ta risasi yakiwa kwenye gari ya Lissu.
Tukio hilo linadaiwa kutokea leo akiwa
nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma ambapo watu hao walimvamia akiwa
kwenye gari kisha kumpiga risasi za miguuni na tumboni. Imeelezwa kuwa
alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, amekimbizwa katika
Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambapo amefikishiwa kwenye chumba cha
upasuaji (theatre) na hali yake ni mbaya sana.
“Ni kweli, Tundu Lissu amepigwa risasi
na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake, amekimbizwa katika Hospitali
ya Mkoa, Dodoma. Na mimi nipo njiani naelekea huko hospitali kumuona,” alisema Mbowe.
Taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.
0 comments:
Post a Comment