Mwenyekiti wa (CHADEMA) Freeman Mbowe amefunguka na kuweka wazi sehemu
alipo dereva wa Tundu Lissu ndugu Simon Mohamed Bakari na kusema kwa
sasa yupo nchini Kenya akipatiwa huduma za kisaikolojia kufuatia
kushuhudia tukio hilo la kinyama.
Mbowe amesema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo
ameweza kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu sakata hilo na kusema kuwa
waliona ni busara kumchukua dereva huyo na kuwa naye nchini Kenya kwa
ajili ya kupatiwa msaada huo hadi watakapooona hali yake ya kiafya na
uhakika na usalama wake ndiyo anaweza kurejea nchini Tanzania.
"Dereva wa Mhe. Lissu, Simon Mohamed Bakari naye tunaye hapa Nairobi
akiendelea kupata huduma za kisaikolojia. Alishuhudia shambulio lile na
aliokoka kimiujiza. Anasumbuliwa na msongo mkubwa wa mawazo. Naye
hatukuona busara kuendelea kumwacha nchini hadi hapo hali yake ya kiafya
na kiusalama itakapohakikishwa. Ni dhahiri kwa aina ya shambulio
lilivyokuwa, wauaji walikusudia kuwauwa wote, Mhe. Lissu na hata Dereva
wake" alisema Freeman Mbowe
Mbali na hilo Mbowe amewataka wabunge wa upinzani kuwa na tahadhari
kubwa akidai kuwa kama wasipokuwa makini huenda kiongozi mwingine
anaweza kupata matatizo kama hayo hata hivyo amesema kuwa tamko la chama
chake litakuja karibuni.
"Tutamuenzi Baba wa Taifa aliyetuasa: “tukiwa waoga tutatawaliwa ma
madikteta!” Wabunge na Viongozi wa Upinzani ndiyo “Target”. Nawasihi
viongozi na wabunge wetu wachukue kila tahadhari. Wanachama nao wawe
tayari kulinda na kupigania wajibu wetu, usalama wa viongozi na chama
chetu kwa ujasiri. Tusipochukua hatua, kesho atadhurika mwingine!Tamko
na agizo rasmi la Chama litafuata karibuni" alisema Freeman Mbowe.
Freman Mbowe amedai kuwa Tanzania si sehemu salama tangu umefanyika
Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 na kudai kuanzia hapo yalianza kujitokeza kwa
mauaji ya viongozi kikiwepo kifo cha Mhe. Alphonce Mawazo Mkoani Geita,
Kupotea kwa kina Ben Saanane. Kutekwa wasanii na kufanyiwa mateso
makubwa pamoja na Wabunge kufungwa na kushtakiwa kila siku
0 comments:
Post a Comment