Home »
» MADINI MAPYA YAGUNDULIWA TANZANIA
Tanzanite
ni madini yanayopatikana Tanzania pekee; madini haya yameipaisha
Tanzania duniani kote na kukuza uchumi wake. Wakati nchi hiyo ikiwa na
madini lukuki ya kila aina leo madini mapya yamegunduliwa katika eneo
lenye madini ya kipekee la Manyara na kupewa jina Merelaniite.
Jina hilo limetokana na eneo ambalo
madini hayo yalipatikana, Merelani (Mererani) katika milima ya Lelatema
katika Wilaya ya Simanjiro huko mkoani Manyara.
Madini
hayo yamegunduliwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha
Michigan cha Marekani, makavazi ya historia asilia ya London, Chuo Kikuu
cha Di Firenze cha Italia na makavazi ya historia asilia ya Smithsonian
ya Washington.
Wataalamu sita waliofanya uchunguzi,
kwenye makala iliyochapishwa kwenye jarida la Minerals (Madini) wanasema
madini hayo yana vipande vinavyofanana na sharubu vya rangi ya kijivu
vya urefu wa milimita moja, ingawa kuna baadhi vyenye urefu wa hadi
mililita 12.
Madini hayo yanakaribiana na madini ya
zoisite (aina ya tanzanite), prehnite, stilbite, chabazite, tremolite,
diopside, quartz, calcite, graphite, alabandite na wurtzite.
0 comments:
Post a Comment