Uongozi
wa Yanga umeonyesha kutofurahishwa na kitendo cha kutoalikwa katika
hafla ya ukabidhi wa vifaa iliyofanywa na wadhamini wa Ligi Kuu Bara,
kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom.
Wakati
wa kukabidhiwa jezi hizo, leo. Yanga haikuwa na mwakilishi na badala
yake, Msemaji wa Simba, Haji Manara akafanya “uchale”, kwenda kuwa
sehemu ya mwakilishi wa Yanga wakati vijana husika wakionyesha jezi za
Yanga za msimu ujao, jukwaani.
Katibu
Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa kuzungumzia hilo amesema wamesikitishwa
na jambo hilo na hasa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi
Tanzania, wameonekana kutowatendea haki.
"Hicho
kitendo kimetusikitisha sana, kiuweli hali hiyo inatufanya tuonekane
wazembe kwa mashabiki wetu kutokana na TFF ambao ndiyo waratibu.
"Niseme
kuwa, TFF haijatupa mwaliko wa aina yoyote ikiwemo email (barua pepe),
simu na hata kutufuata hapa ofisini kwetu maana siyo mbali kutoka hapo
ofisini kwao.
"Kiukweli
kitendo kimetusikitisha sana na kingine ninashangaa hao TFF hizo jezi
zetu wamezitoa wapi? Kwa sababu hizo zilipelekwa kwa mmoja tuliyempa
tenda ya kuziwekea logo, hiyo inamaana waliptia mlango wa nyuma na
kutuzunguka kuchukua jezi bila ya kututaarifu washusika.
"Kitendo
hicho huenda wenyewe TFF wakakiona kidogo lakini kwetu ni kikubwa na
huenda kikaleta mpasuko klabuni kwetu,” alisema Mkwasa akionekana
kutofurahishwa na jambo hilo.
“Kingine
hao TFF kwanini wanapotukata makato yetu wanatoa taarifa, lakini hili
la kukabidhiwa jezi wameshindwa kututaarifu," aliendelea kusisitiza
Mkwasa aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars.
0 comments:
Post a Comment