Raphael Daud ameonyesha kuwa atakuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Yanga.
Hii ni baada ya kucheza dakika 45 zake
za kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Moro Kids ya Morogoro na
kufanikiwa kufunga bao.
Pamoja na kufunga bao, Raphael alionyesha uwezo mkubwa hasa katika kuchezesha timu.
Kiungo huyo kinda aliyejiunga na Yanga
akitokea Mbeya City, alikuwa akitumia muda mwingi kugawa mipira huku
akiomba na kurejesha kwa wenzake.
Pia alikuwa akipiga pasi fupi na ndefu za haraka na kuonyesha kuwavutia wengi.
0 comments:
Post a Comment