Taarifa zilizopo kwa sasa katika mitandao
ya kijamii duniani kote na vyombo vya habari vya Ulaya ni kuhusiana na
ishu ya mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea FC Barcelona Neymar kuhusishwa kukaribia kujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa.
Habari kutoka katika mitandao mingi ya Ulaya inaripoti kuwa PSG hadi sasa wana asilimia 90 ya kumpata Neymar kutokana na mchezaji huyo kuiomba na kuishinikiza Barcelona imuuze, baada ya kocha kumpa ruhusa Neymar na FC Barcelona kuthibitisha Neymar kuombwa kuuzwa.
Lionel Messi ambaye amecheza na Neymar kwa miaka minne toka staa huyo ajiunge na Barcelona, ametumia ukurasa wake wa instagram kumtakia kila la kheri Neymar ambaye leo inaaminika ameshasafiri kuelekea Paris kukamilisha uhamisho huo.
“Ilikuwa ni heshima kushea
chumba kimoja cha kubadilishia nguo na wewe kwa miaka yote hiyo rafiki
yangu Neymar kila la kheri katika hatua mpya ya maisha yako”>>>Messi
0 comments:
Post a Comment