Baada ya headlines zilizochukua nafasi August 1 2017 kuhusiana na beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea club ya Azam FC Gadiel Michael kuripotiwa kuwa anabaniwa na Azam FC kujiunga na Yanga huku Azam FC wakisema hawajapokea ofa kutoka Yanga.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Azam FC Jafari Idd Maganga ameweka wazi kuhusu kinachoendelea kuhusiana na Gadiel Michael na kuhusu habari za Yanga kupeleka barua kwao ya ofa ya kumtaka Gadiel Michael.
“Gadiel bado sana mkataba wake
kuweza kuisha bado miezi sita ili umalizike lakini tuliwaambia Yanga
kama wanamtaka Gadiel waje, jana wamekuja na barua yao ya kumuhitaji
mchezaji na sisi kama Azam FC tumewajibu lakini watafuteni wao waseme
tumewajibu nini” >>> Jafari Iddi
0 comments:
Post a Comment