Home »
» CLOUDS YAMGARAGAZA LADY JAYDEE MAHAKAMANI
Baada
ya kimya cha muda mrefu hatimaye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini
Dar es Salaam, imetoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Clouds Media
Group dhidi ya Mwanamziki mashuhuri hapa nchini Judith Wambura
akifahamika zaidi kama Lady Jaydee.
Itakumbukwa
Kampuni ya Clouds Media Group yenye vituo vya redio na tv zenye
ushawishi mkubwa kwa jamii hapa nchini kupitia kwa Mkurugenzi
wake Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Ruge
Mutahaba walifungua kesi katika mahakama hiyo wakimtuhumu msanii huyo
kuwachafua kupitia blog yake.
Akitoa hukumu hiyo mahakamani hapo hii
leo Hakimu Boni Lyamike amemwamuru Lady Jaydee ambaye alikuwa shahidi
pekee katika kesi hiyo kuwaomba radhi wakurugenzi hao kupitia vyombo vya
habari kwa kuchafua taswira zao huku akitakiwa kuwalipa fidia kutokana
na madhara walioyapata kwa kitendo alichowafanyia ikiwa ni pamoja na
kulipa gharama za wanasheria zilizotumiwa na Clouds Media Group kwenye
kesi hiyo.
Hata
hivyo msanii huyo amekiri kuandika maneno hayo ya kuwachafua mahasimu
wake huku Meneja wake Seven Mosha akinukuliwa na baadhi ya vyombo vya
habari akisema Jaydee atazungumzia hukumu hiyo muda wowote ingawa
kupitia ukurasa wake wa Instagram Jide ameandika “Iam not afraid God is with me all the time”.
0 comments:
Post a Comment