Mnandi
pwani anayeweza kuruka kwa miezi miwili mfululizo aliwahi kuchukuliwa
kuwa ndege mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kuruka lakini baadaye watu
waligundua kuwa barawai mwenye tumbe jeupe (alpine swift) anaweza kuruka
kwa miezi 6 mfululizo. Sasa rekodi hii imevujwa na barawai wa Ulaya.Prof.
Anders Hedenstrom wa Chuo Kikuu cha Lund cha Sweden amegundua kuwa
Barawai wa Ulaya wanatua kwenye nchi kavu kwa miezi miwili tu kila mwaka
ili kuzaliana, baadaye wanaelekea Afrika wakitokea Ulaya ili kupisha
majira ya baridi, halafu wanarudi tena Ulaya kwa ajili ya kuzaliana.
Katika kipindi cha miezi 10 wanapohama, kimsingi hawatui.
Prof. Hedenstrom na wenzake wameweka
vifaa vidogo vya kurekodi data kwa barawai 13 waliokamatwa Kusini mwa
Sweden na kuchunguza hali yao kwa miezi miwili.
Matokeo
yameonesha ingawa barawai wachache waliwahi kutua kwa muda mfupi wakati
wa usiku, au kulala kwa usiku mzima katika majira ya baridi, lakini
muda huo haujafikia asilimia 1 ya kipindi cha miezi 10. Na barawai
wengine hawakuwahi kutua walipohama na kupisha majira ya baridi.
Swali la msingi la kujiuliza hapa ni
ndege hawa wanawezaje kulala? Prof. Hedenstrom amesema anakadiria kuwa
ndege hao huenda wanaweza kulala huku wakiruka kama mnandi pwani
wanavyofanya.Unaweza
kufikiria kuwa ndege hao wanaishi maisha magumu kwa sababu wanaruka kwa
muda mrefu sana, lakini ndege hao wana umri mrefu. Barawai mwenye umri
mkubwa zaidi aliishi kwa miaka 20. Prof. Hedenstrom amesema umbali
anaosafiri ndege mwenye umri huo ni sawa na kwenda mwezini na kurudi
duniani mara 7. Hii ndio dunia ambayo ni zaidi ya uijuavyo.
0 comments:
Post a Comment