Denis Massawe
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng.
Gerson Lwenge amezitaka wilaya zote nchini kujenga mabwawa ya kuvuna
maji ya mvua ili kukidhi mahitaji ya maji hasa nyakati za ukame na
kuwezesha kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yao.
Akizungumza
na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi
wa Kongamano la Wadhibiti wa Huduma za Maji Kusini na Mashariki mwa
Afrika (ESAWAS), Eng. Gerson Lwenge amesema Mabwawa hayo yatasaidia
kupatikana maji hasa vipindi vya ukame na maeneo ya vijijini ambako
hakuna miundombinu ya maji safi na salama.
Naye
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Mbogo Futakamba
amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza kwa kiwango kikubwa
kwenye sekta ya maji ambapo mpaka sasa imekwishakamilisha ujenzi wa
mtambo wa maji wa Ruvu chini unaosambaza zaidi ya lita za maji milioni
200 kwenye Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwa
upande wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi amesema kuwepo kwa
vyombo vya udhibiti wa huduma za maji kama vile ESAWAS vitasaidia
kuondoa migogoro kati ya watumia maji na watoa huduma za maji.
0 comments:
Post a Comment