Denis Massawe
Pambano la ngumi kuwania ubingwa wa
dunia wa uzito wa juu linalotambuliwa na WBA lililotarajiwa kupigwa
Desemba 10 ndani ya Manchester Arena liliahirishwa baada ya Wladimir
Klitschko kuwa majeruhi akisumbuliwa na kiazi cha mguu.
Baada ya kuarishwa kwa pambano hilo,
Shirikisho la masumbwi duniani WBA limethibitisha kuwepo kwa pambano
hilo mwakani kati ya mwezi Machi na April huku Joshua akipata kibali cha
kupigana na Eric Molina mwezi Desemba.
Promota wa Klitschko Bernd
Boente ameeleza kuwa yeye na timu nzima ya Klitschko wamefurahishwa na
maamuzi ya WBA ambayo yamezingatia afya ya bondia wao.
Klitschko ambaye
ni bingwa wa zamani wa dunia amepigana mapambano 68 akishinda 64 na
kupoteza 4 huku 53 akishinda kwa KO. Anthony Joshua mwenye miaka 27 hadi
sasa ameshapigana mapambano 17 ya uzani wa juu na kushinda yote kwa KO.
0 comments:
Post a Comment