Moto ulivyoteketeza Soko la Sido, Mbeya.
Natoa pole kwa wote walioathirika na
janga la moto kwa wafanyabiashara soko la Sido. Soko la Sido lilianza
kuungua saa 21.32 Hrs jana usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara
wa soko la sido.
Pamoja na kutoa pole niwashukuru
wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano na kazi kubwa ya kudhibiti
moto usiendelee kuleta madhara makubwa zaidi.
Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Mbeya imeunda kamati ya kufanya tathmini ya kujua hasara na chanzo cha Moto huo .
Tunaomba wananchi waendelee kuwa
watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo
cha moto na hasara iliyopatikana
Aidha vyombo vya ulinzi vinaendelea
kuchunguza kujua kama moto huo utakuwa umesababishwa na mtu/watu
uchunguzi huo bado unaendelea
Nirudie tena kuwapa pole wote walioathirika na janga na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu
Amos G.Makalla
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
0 comments:
Post a Comment