Picha na maktaba.
ROMBO: Waumini wawili wa Kanisa Siloam wamekufa maji wakibatizwa katika Mto Ungwasi wilayani Rombo baada ya mmoja wao kupandisha mapepo na kuwatumbukiza majini.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani
Kilimanjaro, Agnes Hokororo amethibitisha tukio hilo lililotokea, Julai
16 saa sita mchana. Ubatizo huo ulifanyika kwenye kina kirefu cha mto
huo. Amesema wakati ibada ya ubatizo mmoja wa waumini aliyepandisha
mapepo alimtumbukiza mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri kubatizwa na
mchungaji.
Hokororo amesema muumini mmoja
alipoona mwenzake ametumbukizwa majini aliamua kumwokoa, ndipo
aliyepandisha pepo alipowashikilia wote wawili ndani ya maji na
kuwasababishia kifo.
Amesema watu watatu akiwamo mchungaji wa kanisa hilo lililopo katika Kijiji cha Mandechini wanashikiliwa.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment