Mbunge Gulamali (kulia) akiwa na Sanjay.
Msanii mkongwe wa filamu kutoka India (Bollywood), Sanjay Balraj Dutty, ametua nchini hivi karibuni na kupokelewa na Mbunge wa Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Seif Khamis Gulamali (CCM) tayari kwa ziara yake ya kutembelea vivutio vya utalii.
Imeelezwa kuwa ameanza kwa kutembelea na kupumzika katika mbuga ya wanyama ya Ngorongoro.
Wakiteta jambo.
Sanjay ambaye wazazi wake pia walikuwa
nguli wa Bollywood, Sunil Dutt na Nargis Dutt, alizaliwa Julai 29 mwaka
1959. Mbali na uigizaji pia ni producer mzuri wa filamu hizo.
Sanjay amewahi kucheza filamu zaidi ya
100 tangu mwaka 1981 alipoanza uigizaji rasmi, hasa akibeba uhusika wa
kimapenzi na uchekeshaji (komedi).
Sanjay akipokelewa na Gulaman.
Katika miaka 35 ya uigizaji, Sanjay
amewahi kutwaa tuzo lukuki zikiwemo Filmfare Awards (mbili), IIFA
Awards, Bollywood Movie Awards (mbili), Screen Awards (tatu), Stardust
Awards (tatu), Global Indian Film Award (moja) na Bengal Film
Journalist’s Association Award (moja). Filamu zake nne zilishinda
vipengele mbalimbali vya National Film Awards.
0 comments:
Post a Comment