Shabiki wa klabu ya Yanga akibebwa na msalaba mwekundu baada ya kupoteza
fahamu.
Miongoni mwa mambo yenye uwezo mkubwa wa kuleta furaha ama huzuni
iliopitiliza katika maisha ni ushabiki wa kupitiliza wa mchezo wa mpira wa
miguu.
Na hili limejizidhirisha baada mkazi mmoja wa mtaa wa Mianzini, Mbagala,
jijini Dar es Salaam Mzee Njimbwi kufariki dunia Jumapili iliyopita.
Sababu inayosadikika kuchukua uhai wake ni furaha aliyokuwa nayo baada ya
timu ya Dar Young African maarufu Yanga, kunyakua ushindi wa magoli
2-1 dhidi ya Mbeya City uliyoifanya Klabu ya Yanga kufikisha pointi 65 sawa na
mahasimu wao Simba Spot Club huku ikiongoza ligi kwa wastani wa magoli ya
kufunga na kufungwa.
Yanga ilianza kupata goli la kwanza dakika ya Saba kipindi cha
kwanza mfungaji akiwa ni Simon Msuva, ambaye aliunganisha kwa kichwa mpira wa krosi
uliopigwa na Hassan Hamisi Ramadhani ‘Kessy’.
Mbeya City walisawazisha goli hilo dakika ya 58 kupitia Haruna
Shamte, baada ya kazi kubwa kufanywa na Ditram Nchimbi, kisha Shamte
kutumbukiza mpira huo nyavuni.
Obrey Chirwa ndiye aliyeipatia timu ya Yanga ushindi, baada ya kuunganisha
kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Juma Abdul.
Ushindi huo wa klabu ya Yanga ulimfanya mzee Njimbwa kushindwa
kuvumilia furaha yake wakati akiwasimulia washabiki wenzake kijiweni siku ya
Jumapili Asubuhi, hivyo wenzake waliokuwa nae walishangaa kumuona mzee huyo akidondoka
chini na kufariki papo hapo.
Kufuatia kifo hicho cha mzee Njimbwa kinadhihirisha kabisa jinsi
ushabiki wa mchezo wa mpira unavyoshabihiana na sumu tena ya panya kwani ili
lidhihirike hili, jaribu kuwa shabiki wa mpira halafu timu yako ishindwe ndo utajua
ukweli wa tukio hili.
mashabiki wa Yanga wakiwawamepoteza fahamu
Maumivu yatokanayo na
ushibiki ndiyo yaliyoondoa uhai wa mzee Njimbwa ama waulize mashabiki wa simba au Arsenal
watakuelezea vizuri sana.
Mzee Njimbwa anamfuata Mkenya, Suleiman Alphonso Omondi,
aliyejinyonga miaka sita iliyopita baada ya Arsenal kutolewa nje ya michuano ya
klabu bingwa za Ulaya (Champions League), kwa kudundwa mabao 4-1 na wapinzani
wao wa kijadi Manchester United.
Uadui kati ya Arsenal na Manchester United ulianza toka mwaka 1919
na ukalipuka upya miaka ya 1990, wakati wa meneja Alex Ferguson na Arsene
Wenger na umahiri wa manahodha wa klabu hizo Roy Keane (Man U) na Patrick
Vieira (Arsenal).
Kipindi Arsenal ikiwika kati ya mwaka 2000 na 2005, kiasi cha
kuitwa ‘Invisibles’ ambapo mwaka 2003-
2004 ilimaliza ligi nzima bila kufungwa na timu yeyote.
Sasa mwaka 2009, Mkenya Omondi alighadhabika aliposhuhudia
Arsenal ikimwagiwa pilipili machoni katika fainali hizo, waliomshuhudia dakika
za mwisho wanasema baada ya kubaini Arsenal imetolewa, hayati Omondi
alitoka nje ya Bar ya Bamba, Embakasi, Nairobi, akitokwa machozi.
Kesho yake maiti ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 ilikutwa
ikining’inia barazani, masikini Omondi alijiua akiwa amevaa jezi ya Arsenal.
Kifo ni miongoni mwa matokeo ya ushabiki uliopiliza na kama
ushabiki ukikukosa kwenye kifo basi hupelekea kuwa chizi ama mwendawazimu
kabisa si wa kuokota makopo bali wa kimpira yaani kufanya vitu ambavyo kitafsiri
vinaonesha kuwa umependa mpaka umeloweya.
0 comments:
Post a Comment