INAUMA sana. binti mmoja mmoja aliyejulikana kwa jina la Joyce Joseph
(18), mkazi wa magu mkoani mwanza, yuko kwenye kipindi kigumu cha
mateso na maumivu ya ugonjwa wa kansa ya ngozi huku akiwa ametimuliwa
katika nyumba aliyokuwa anaishi.
Joyce Joseph akiweka pozi.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Joyce alianza kusimulia historia
yake ya maisha kwa kusema, awali alikuwa akiishi kama mmoja wa watoto
katika familia ya mama Mayeji lakini baadaye alianza kunyanyaswa baada
ya kuanza kuumwa.
Ngozi ilivyodhurika.
“Mimi niliokotwa nikiwa mtoto mdogo wa siku mbili ambapo mama huyu
niliyekuwa naishi naye alikuwa akienda kuuza nyanya sokoni akanikuta
nimetupwa kwenye mfuko wa rambo ndipo aliponiokota na kuanza kunilea
kama mtoto wake bila mimi kutambua chochote,” alisema Joyce.
Akisimulia zaidi kwa uchungu, alisema baadaye alikuja kugundua kuwa
si mtoto wa familia hiyo pindi alipoanza kuugua ugonjwa wa kansa akiwa
na umri wa miaka 10.
Nywele na shingo vilivyoathirika.
Alisema alipoanza kuugua, alianza kutokwa na vipele kama ugonjwa wa
tete kuwanga mwilini ambapo alianza kujikuna kila mara na vipele hivyo
vikawa haviponi. “Yaani nilikuwa najikuna kweli mwili mzima lakini cha
ajabu kila nilipokuwa nikivipasua vipele hivyo, vililikuwa haviponi
jambo ambalo lilinifanya nihisi kuwa nina tatizo mwilini,” alisema
Joyce.
Binti huyo alisema mama huyo alikuwa akijaribu kumpeleka katika
hospitali mbalimbali kutafuta tiba lakini kila alikoenda, hakupata tiba
sahihi lakini kilichomuuma zaidi, baba wa familia hiyo akaanza
kumnyanyapaa kwa kumpiga na kumtenga na watoto wengine. “Niliumia sana. Baba badala ya kumsaidia mama, akaanza kuninyanyapaa.
Joyce akiweka pozi.
Hapo ndipo nilipojua sasa kumbe mimi si mtoto wa familia hiyo baada
ya baba kuanza kunipiga kila mara bila kosa lolote na kutufukuza mimi na
mama mpaka kufikia hatua ya kumvunja mkono mama na kumwambia kuwa
anahangaika na mimi wakati siyo mtoto wake,” alisema Joyce.
Joyce aliendelea kuzungumza kuwa, mama huyo aliendelea kuhangaika
naye wakati mwingine naye akawa anampiga na kujikuta akikosa msaada
hivyo kuamua kutoweka nyumbani hapo na kuanza kuwa analala mitaani mpaka
alipokutana na msamaria mmoja aliyemshauri kwenda kuonana na Flora Lauo
kupitia taasisi yake ya Nitetee ambaye ndiye aliyegundua kuwa ana
tatizo la kansa ya ngozi.
Akiwa na familia yake.
“Nilikutana na msamaria mmoja ndiyo akanishauri niende kwa Flora
Lauo. Nashukuru Mungu alinipokea, na ndipo nilipopima na kugundulika
kuwa nina kansa ya ngozi, nimeanza matibabu katika Hospitali ya Bugando
lakini kiukweli bado nahitaji fedha kwa ajili ya matibabu,” alisema
Joyce.
Kwa yeyote aliyeguswa na tatizo la Joyce, tafadhali anaombwa
kumchangia chochote alichonacho ili aweze kuendelea na matibabu zaidi
kupitia simu yake ya mkononi; 0752 675883.
SOURCE: RISASI
0 comments:
Post a Comment