Uwezo wa watu kuishi unategemea
namna ya utajiri au uwezo wa kifedha waliokuwa nao. Wanavyoingiza fedha
zaidi ndivyo wanavyozidi kubalika katika namna ya kuishi. Wapo matajiri
ambao hujenga nyumba ambayo kutokana na ukubwa wake inaweza kuishi hadi
watu 100 na huwatumia wabunifu wa hali ya juu…
Hii hapa Top Ten ya nyumba ghali zaidi za Mabilionea
10: 360 Mountain Home Road
Nyumba hii ipo Westside, California,
Marekani na inamilikiwa na Masayoshi Son, CEO wa Softbank. Kasri hili
limejengwa kwa namna yake likiwa na bwawa na kuogelea la futi 1.117,
uwanja wa tennis, Maktaba. Kwa sasa linakadiriwa kuwa na thamani ya
Dollar Milioni 117.5 zaidi ya Tsh. Bilioni 258.
9: Xanadu 2.0
Hii inapatikana Seattle, Washington na
inamilikiwa na Bill Gates, mwasisi-mwenza na Mwenyekiti wa Microsoft.
Lina eneo la futi 66,000 likisanifiwa kwa mtindo wa Pacific lodge
lina
maktaba binafsi, chumba cha chakula, bwawa la kuogelea ambalo lina
mfumo wa muziki chini (swimming pool with underwater music system).
Linakadiriwa kuwa na thamani ya Dollar Milioni 120.5 zaidi ya Bilioni
264.
8: Blossom Estate
Ukitembelea Palm Beach, Florida,
utakutana na kasri hili ambalo linamilikiwa na Kenneth Griffin, Mwasisi
na CEO wa Citadel LLC. Jengo kwenye ekari 8 ambalo linajumuisha nyumba
nne zinazojitegemea katika eneo ambapo tatu kati ya hizo zinaangalia
ufukwe. Lina thamani ya Dollar Milioni 130 zaidi ya Tsh. Bilioni 286.
7: Ellison Estate
Jumba hili linapatikana Woodside,
California, ni milki ya Tajiri namba tatu katika nchi ya Marekani, Larry
Ellison, mwasisi-mwenza wa Oracle Corporation. Kuna majengo 10 ndani ya
ekari 23, bwawa la samaki, Ziwa lililotengenezwa, chumba cha chai, na
nyumba ya bafu ambayo imesanifiwa kwa mtindo wa Kijaan. Thamani yake ni
Dollar Milioni 200 zaidi ya Tsh Bilioni 440.
6: One Hyde Park
Nyumba ya ukubwa wa futi 25,000 ambayo
ipo katika jiji la London, inamilikiwa na tajiri wa Ukraine, Rinat
Akhtemov. One Hyde Park ni moja kati ya makazi maarufu sana United
Kingdom. Thamani yake ni Dollar Milioni 213 zaidi ya Tsh. Bilioni 468.
5: 18-19 Kensington Palace Gardens
Nayo pia iko katika jiji la London,
ikimilikiwa na Lakshmi Mittal, mmilikiwa wa viwanda vya kutengeneza
chuma wa India. Ina vyumba 12 vya kulala, bafu la Kituruki, eneo la
kuegesha magari zaidi ya 20. Wakati wa kununuliwa ilikuwa ndiyo nyumba
iliyouzwa kwa bei ya juu zaidi Duniani. Awali lilimilikiwa na Berne
Ecclestone, Mkuu wa Formula One ambapo thamani yake kwa sasa ni Dollar
Milioni 222 ambazo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 488.
4: Four Fairfield Pond
Hii ipo Sagaponack, New York na
inamilikiwa na Ira Rennert, mwekezaji wa Marekani na Mfanyabiashara.
Jumba hili lina vyumba 29 vya kulala, mabafu 39, na mabwawa 3 ya
kuogelea na umeme wa kijitegemea. Thamani yake ni Dollar Milioni 248.5
zaidi ya Tsh. Bilioni 545.
3: Villa Leopolda
Kasri hili lipo Villefranche-sur-Mer,
Ufaransa, likienea katika eneo la ukubwa wa ekari 18 na lilitumika kama
makazi ya King Leopold II wa Ubelgiji lakini sasa linamilikiwa na
Mbarazil Lily Safra ambaye amerithi baada ya kifo cha mumewe Edmond
Safra. Thamani yake ni Dollar Milioni 750 zaidi ya Tsh. Trilioni 1.65.
2: Antillia
Linajulikana pia kama ‘One Billion
Dollar home’, lipo katika eneo la ukubwa wa square foot 400,000 katika
mji wa Mumbai, India na linamilikiwa na Bilionea Mukesh Ambani. Kutokana
na ukubwa wake linahitaji watu 600 kulihudumia. Kama linavyoitwa jumba
hili lina thamani ya Dollar Bilioni 1 zaidi ya Tsh. Trilioni 2.2.
1: Buckingham Palace
Kasri linamilikiwa na familia ya
kifalme na kwa sasa lina thamani ya Dollar Bilioni 1.55 zaidi ya Tsh.
Trilioni 3.3. kasri hili lina jumla ya vyumba 775.
0 comments:
Post a Comment