Friday 18 August 2017

HIZI NDIYO PICHA BORA ULIMWENGUNI KUWAHI KUPIGWA

Najua wengi niwapigaji picha lakini wapo bora zaidi. Na ili kudhihirisha hilo ndiyo maana nimekuwekea listi nzima ya picha zilizotajwa kuwa bora na mtandao wa Funbiz.

Naamini  Mdau wangu utafurahia tena hasa kama unandoto ya kuwa mpiga picha bora.

Miongoni mwa picha zilizotikisa ulimwengu ni hii ambayo ilipigwa na mwandishi mahiri nchini India, Yawar Nazir, mnamo septemba 30 mwaka 2014. ikionesha mbwa mwenye masikitiko makubwa akiwa nje ya nyumba ilibomoka kwa kile kilichonekana kuwa chanzo ni mafuriko.
Picha nyingine iliyoonekana kuwa mwiba mkali ulimwenguni ni hii iliyopigwa na Mwandishi Vasil Fedosenko wa Reuters. iliyokuwa ikionesha walinzi wa serikali wakitupiwa mabomu ya moto wakati wa madai ya uhuru Kiev.
Nyingine ni hii ya mwandishi mahiri, Pablo Blazquez, aliyopiga baada ya Ng'ombe dume kumpiga refa wa mashindani ya wanyama hao wakati wa tamasha lao huko Pamplona, nchini Hispania.
Ambapo nchi ya hispania huwa na tamasha la ng'ombe ambalo hujulikana kama Bulls Festval kila Julai 14.
Huwezi taja picha bora bila kuanza kutaja hii ambayo ilipigwa na Mwandishi hatari kuwahi kutokea, Robertus Pudyanto, huko Malang, Indonesia, baada ya kumuotea mwanamama Mulan Jamilah, akimchapa busu chui mwenye miaka 6 katika gadeni iliyo jirani na nyumba yake.
Nyingine iliyotikisa ni ya mwandishi wa Reuters, Damir Sagolj, ambaye aliweza kuipiga picha ipasavyo ya wapigania demokrasia ambayo waliamua kuandamana wakiwa wamejifunika miavuli huko Hong Kong Octoba 28, mwaka 2014.
Nyingine ni hii ya mwandishi mahiri wa ZumaPress, Thomas Geyer, ambayo alifanikiwa kuwapiga picha Vivian Boyack(kushoto) na Alice Dubes (katikati) wakifungishwa ndoa na Rev. Linda Hunsaker, baada ya kukaa katika mahusiano kipindi cha miongo saba.
ambapo Boyack akiwa na miaka 91 huku Dubes akiwa na miaka 90.
Nyingine ni hii ya mwandishi wa EPA, Felipe Trueba, aliyopiga watu wawili waliyokuwa wakikatiza katika barabara ilipasuka ikitenganisha kati ya eneo la Iquique na Alto Hospicio, nchini Chile Aprili 3, mwaka 2014.
kubwa ni hii iliyopigwa na mwandishi wa Reuters, Luke MacGregor, ikimuonesha mtu mfupi zaidi duniani, Chandra Bahadur Dangi akiwa na mtu mrefu zaidi duniani Sultan Kosen, katika siku ya kumbukumbu Duniani iliyofanyika Londoni, Novemba 3, Mwaka 2014.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive