Pemba. Yanga imetakiwa kuwa makini na safu yao ya ulinzi inayoonekana kutokuwa sawa wakiambiwa endapo wasipofanya hivyo watajikuta katika mazingira ya mbele ya Simba.
Kauli hiyo imetolewa na kocha Mzee Abdallah mwenye leseni B ya ukocha wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ameiambia MCL Digitala kuwa Yanga wana kikosi imara ili ubora wao mkubwa upo katika safu ya kiungo na ushambuliaji.
Abdallah amesema kocha wa Yanga, George Lwandamina endapo anataka kuifunga Simba anatakiwa kuhakikisha anaisuka vyema safu yake ya ulinzi ambayo imeiona bado ina mapungufu kiasi ambayo yanaweza kuwaghalimu endapo watakutana na Simba wakiwa hivyo.
Alisema endapo mabeki hao wa Yanga kwa mtindo wanaocheza wakakutana na washambuliaji na viungo wenye mbio wanaweza kujikuta wakifanya makosa makubwa yanaweza kuwaghalimu ambapo wakirekebisha hilo kila kitu kwao kiakuwa rahisi Agosti 23.
"Nimepoteza dhidi ya Yanga matokeo nimeyakubali, tulijiandaa vyea kuwazuia, lakini niseme wenzetu walikuwa bora zaidi yetu wameonyesha kwamba wako sawa najua kwamba wanajiandaa na ligi na kucheza dhidi ya Simba,"alisema Abdallah
"Tofauti na nilivyokuwa nawajua jana tumeona Yanga wakibadilika katika mbinu wakicheza soka la kwenda mbele zaidi wasiwasi wangu ni safu yao ya ulinzi naona bado haijawa katika kiwango bora kuna kazi kocha wao anatakiwa kuifanya wakikutana na timu yenye wasambuliaji wenye kasi wanaweza kupata shida.
0 comments:
Post a Comment