Robert Mugabe alijiuzulu Novemba 21
baada ya kuahidiwa kinga ya kutoshtakiwa, kulipwa dola za Marekani 10
milioni kwa mkupuo, mshahara wa kila mwezi, matibabu, usalama wake
pamoja na ulinzi wa mali zake, gazeti la Independent limeandika.
Uchunguzi uliofanywa na Independent umefichua kwamba watu wa Mugabe walioshiriki katika mazungumzo yaliyowezesha yeye kuondoka walifanikiwa kufikia makubaliano na majenerali kuhakikisha mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 93 haendi kuishi uhamishoni bali afurahie kustaafu kwake nchini Zimbabwe na apate marupurupu yake.
“Serikali itamlipa Mugabe dola 5 milioni kwa mkupuo na kisha kiasi kinachosalia atakuwa akilipwa kwa mafungu,” chanzo kimoja kimesema. “Mugabe atapatiwa matibabu pamoja na mshahara kamili kila mwezi. Na ikiwa atafariki mkewe atakuwa analipwa nusu mshahara kila mwezi.”
Mugabe alifanya majadiliano ili aweze kuondoka salama kupitia timu ya wapatanishi ambayo ilijumuisha kasisi wa Kikatoliki, Fidelis Mukonori na gavana wa zamani wa RBZ Gideon Gono. Mukonori alisema katika mahojiano kwamba wajibu wake ulikuwa kuwa mpatanishi kati ya majenerali na Mugabe.
0 comments:
Post a Comment