NYOTA wa soka wa klabu ya Real Madrid ya Hispania
na timu ya taifa ya Wales, Uingereza, Gareth Bale, ameripotiwa kumtaka
staa wa muziki Mmarekani, Beyonce, kutumbuiza siku ya harusi yake mwaka
kesho.
Hata hivyo, itambidi Bale zimtoke Paundi milioni l.5 (Sh. bilioni 4.4) ili kupata burudani ya nyota huyo maarufu duniani.
Bale anategemea kumwoa mpenzi wake wa siku
nyingi, Emma Rhys-Jones, ambapo anataka mwanamuziki huyo wa kundi
lililokuwa linajulikana kama Destiny’s Child, awaburudishe waalikwa.
Ndoa hiyo iliyotakiwa kufanyika nchini Italia
mapema, ilichelewa kutokana na baba wa Rhys-Jones kufungwa kutokana na
utapeli nchini Marekani.
Wawili hao wamefahamiana tangu utotoni na
wanaishi jijini Madrid na watoto wao wa kike wawili. Baada ya sherehe
hiyo huko Italia, wamepanga kufanya sherehe nyingine huko Wales.
Bale ana mkataba na Real Madrid ambapo analipwa
Sh. milioni 894 kwa wiki (Paundi 300,000) na anasemekana anaweza kuhama
kwenda Manchester United ya Uingereza. Beyonce, aliyeoana na nyota wa
muziki wa hip-hop, Jay-Z mwaka 2008, ameuza rekodi zipatazo milioni 100
akiwa msanii anayejitegemea.
0 comments:
Post a Comment