Friday, 8 September 2017

TSHISHIMBI AITIKISA NJOMBE

 
Njombe Mji na Yanga zinatarajiwa kupambana keshokutwa Jumapili ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo Tshishimbi tayari ameshajizolea umaarufu kutokana na kiwango kikubwa alichokionyesha kwenye mechi yake ya kwanza hapa nchini dhidi ya Simba katika Ngao ya Jamii.  

JEZI za kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi tayari zimeanza kuuzwa kwa kiwango cha juu mkoani Njombe ikiwa ni siku chache kabla ya Yanga haijacheza na Njombe Mji kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani humo. 
Jana Alhamisi,  tulizipata picha mbalimbali zikionyesha wafanyabiashara wa jezi katika Stendi Kuu ya Mabasi Njombe. 

Licha ya kuwepo kwa jezi nyingi za wachezaji mbalimbali wa Yanga, lakini zenye jina la Tshishimbi raia wa DR Congo, ndizo zilikuwa nyingi huku ikisemekana kwamba ndizo zilizokuwa zikinunuliwa kwa wingi. 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive