Kiungo wa Yanga, Pius Buswita ameamua kuwapotezea
wanaomponda kwa sababu ya tukio lake la kusajili timu mbili na sasa
ameelekeza nguvu zake ndani ya kikosi chake kuhakikisha anapata nafasi
ya kudumu kikosi cha kwanza.Kiungo huyo aliyeichezea Mbao FC msimu
uliopita, baada ya tukio hilo, alipata adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja,
lakini, baadaye aliachwa huru kwa sharti la kurudisha pesa za Simba
ambazo ni Sh10 mil.
“Sipendi maneno, ndiyo maana nimeamua kujifanya kama sisikii vile yote wanayosema, kweli tatizo lilitokea lakini wanachokizungumza ni tofauti na ilivyo, wanasema nawatukanisha mawakala lakini ukweli naujua mwenyewe,”alisema Buswita bila kufafanua kwa undani akisitiza tatizo limeshakwisha.
“Sasa natizama yaliyo mbele yangu, nahitaji kuisaidia Yanga kupata mafanikio, japo kuna changamoto ya namba lakini nitapigania nafasi ili nicheze kikosi cha kwanza.”

0 comments:
Post a Comment