YANGA sasa imekamilika kwani kesho Jumapili mshambuliaji wake, Obrey Chirwa anatarajiwa kuanza kucheza dhidi ya Njombe Mji na imethibitishwa yupo fiti kufanya kazi yake.
Chirwa raia Zambia hakuichezea Yanga mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara
dhidi ya Lipuli FC ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kesho Jumapili, Yanga itacheza na Njombe Mji mechi ya pili ya ligi
hiyo kwenye Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe na Chirwa anatarajiwa
kucheza kwani amepona majeraha ya mguu.
Akizungumza na Championi Jumamosi kutoka Njombe,
Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh alisema; “Wachezaji wote wapo vizuri
akiwemo Chirwa ambaye tunatarajia ataanza kwani yupo fiti lakini kocha
ataamua.
“Kikosi chetu kipo vizuri kuelekea mchezo huo, kuhusu afya ya Chirwa
yupo vizuri na kama mambo yakienda vizuri anaweza kuanza na kufanya kazi
yake kama kawaida.”
Hafidh alisema Amissi Tambwe, Buruhan Akilimali na Beno Kakolanya wao
wameachwa jijini Dar es Salaam kwani ni majeruhi lakini watajiunga na
wenzao watakaporejea.
0 comments:
Post a Comment