HALI
ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye juzi
Alhamisi alishambuliwa kwa risasi mjini Dodoma na watu wasiojulikana,
imeelezwa amepelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) baada ya
kufanyiwa upasuaji wa awali huko Nairobi, Kenya.
Lissu
ambaye aliwahi kusema kuwa yeye ni shabiki wa Yanga wakati alipokuwa
akizungumza na Moja ya vyombo vya habari hapa nchini na kudai tangu mwaka 1993 hajawahi
kwenda uwanjani, alikumbwa na balaa hilo la kupigwa risasi tumboni na
miguuni majira ya saa 7:00 mchana nyumbani kwake Area D baada ya
kuegesha gari akitokea bungeni.
Kutokana
ha tukio hilo, baadhi ya wachezaji wa zamani wa Simba na Yanga
wameonyesha kusikitishwa vilivyo na kujikuta wakitoa yao ya moyoni.
Akizungumza
kwa niaba ya wachezaji wa zamani wa Yanga, nahodha wa zamani wa timu
hiyo, Sekilojo Chambua alisema: “Hakika tukio hilo limetusikitisha sana
kwani siyo la kiungwana.
“Tuko
hilo ambalo limetokea mchana kweupe kabisa hakika si jambo zuri hata
kidogo, tunapaswa kulikemea vikali kwani mambo kama hayo siyo utamaduni
wetu.”
Naye
mchezaji wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa, alisema: “Tukio hili
limetuacha na maswali mengi juu ya watu hao ambao wamekuwa wakifanya
matukio hayo na hawajulikani.
“Tunapaswa kukemea vikali matukio haya, tuwe na kampeni ya kukemea mambo kama haya kwa ajili ya kulinda heshima ya nchini yetu.”
Kwa
mujibu wa Chadema, jana majira ya saa 10 alasiri, Lissu alitolewa
‘theatre’ alikokuwa anafanyiwa upasuaji wa saa saba akitolewa risasi.
Jana
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, alilaani tukio hilo na
kuitaka serikali kukomesha vitendo vya watu wasiojulikana kufanya
matukio hatarishi
0 comments:
Post a Comment