IMEBAINIKA
kuwa mkataba wa kipa, Aishi Manula ndani ya klabu ya Simba ndiyo
uliochangia timu hiyo kuachana na kipa Mghana, Daniel Agyei.
Beki
wa kati wa Azam FC, Yakubu Mohammed ameiambia Mwanaspoti kuwa walimsihi
Manula asiende Simba kwani angeshindwa kutamba mbele ya Agyei lakini
aling'ang'ania kwa kuwa alifahamu mpinzani wake huyo ataondolewa.
"Agyei
ni kipa makini, hata rekodi zake zilikuwa vizuri. Tulipoona Manula
anakwenda Simba tulimshauri asiende kwani angepata ushindani mkubwa
kutoka kwake, nadhani alifahamu kwamba ataondolewa," alisema Mohammed.
"Kama
Agyei angebaki ushindani ungekuwa mkubwa zaidi, Simba pia wangekuwa
vizuri zaidi. Kwa sasa Manula ana uhakika wa kuanza kila mechi,"
alifafanua.
0 comments:
Post a Comment