Tuesday 5 September 2017

TSHABALALA ATUMA UJUMBE AZAM FC

MLINZI wa kushoto wa Simba na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ maarfufu Zaidi Tshabalala amefungukwa kuwa mchezo wao wa wikiendi hii mbele ya Azam utakuwa mwepesi kwao kuibuka na pointi tatu kutokana na malengo ya kupata pointi mbele ya timu yoyote ile waliyojiwekea.

Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Azam kwenye pambano la ligi kuu ambalo litapigwa Jumamosi hii katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar, ambapo mchezo baina ya vikosi hivi viwili utakuwa wa kwanza kupigwa katika uwanja huo.

Akizungumza  Tshabalala amesema kuwa licha yakutambua ugumu waliokuwa nao Azam lakini jambo hilo haliwazuii wao kuibuka na pointi kama ambavyo wamepania kufanya hivyo kwenye kila mchezo wao ambao wataucheza msimu huu.

“Azam wagumu kwa wengine lakini kwetu watalainika tu kwa sababu hii siyo mara ya kwanza tunakutana nao na tunawajua vizuri jinsi ambavyo wamekuwa wakicheza, kwamba tutumie mbinu gani kupata pointi na kizuri zaidi ni kwamba tumekusanya nyota wao ambao walikuwa tishio kwetu kwenye misimu kadhaa nyuma.

“Unajua nina uhakika mkubwa wa kushinda mechi hiyo kwa sababu ya malengo yetu ya mwaka huu ya kupata pointi haijalishi tunacheza na mpinzani gani awe mdogo au mkubwa, kitu cha muhimu na kwanza ni kushinda na kupata pointi na siyo jambo lingine lolote lile,” alisema Tshabalala.   
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive