KOCHA Mkuu wa timu ya Njombe Mji, Hassan Banyai baada ya kupoteza dhidi ya Prisons kwa bao 2-1 ameibuka na kusema kuwa licha ya kuwaheshimu Yanga kama timu kongwe lakini hawatakubali kupoteza dhidi yao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Banyai amesema wanajua kama michezo ya ligi kuu ni migumu lakini hatakubali kupoteza tena dhidi ya Yanga japo ni timu kubwa na wanaiheshimu.
“Tunajua kuwa Yanga ni timu kubwa na tunaiheshimu lakini niwaambie tu watatusamehe kwani hatutokubali kupoteza kwa mara ya pili licha ya ligi kuu bara kuwa na michezo migumu kwani kila timu wanataka ushindi hili waweze kusonga mbele,” alisema Banyai.
0 comments:
Post a Comment