Sakata la kiungo mshambuliaji Pius Buswita kufungiwa, ni kama vile
limemalizika na mchezjai huyo atakuwa na nafasi ya kuichezea Yanga kama
alivyotaka.
Awali mchezaji huyo alidai sheteni alimpitia na akajikuta akisaini mikataba miwili katika klabu za Simba na Yanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, Elias
Mwanjala amelizungumza hilo leo Jumatano kwa kusema klabu hizo mbili
zimezungumza na kuafikiana juu ya mchezji huyo ambapo Yanga ikikamilisha
kile walichozungumza, rasmi Buswita atakuwa mchezaji wa Yanga.
Mwanjala amesema kuwa baada ya Simba na Yanga kukubaliana juu ya
mchezaji Pius Buswita ili atoke kifungoni, Yanga itatakiwa kuilipa Simba
shilingi milioni 10 ambazo Buswita alizichukua aliposaini Simba.
Amesema kuwa muda wowote fedha hizo zikilipwa basi Buswita
ataruhusiwa kucheza, jambo ambalo linaonekana kuwa ni dogo kwa Yanga
kulitekeleza.
0 comments:
Post a Comment