SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa anaweza kumpiga marufuku Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kuongea bungeni kwa kipindi chote cha Bunge la 11 na kwamba hana cha kumfanya.
Jana Ndugai alimpeleka Zitto Katika Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa kulidharau Bunge.
Akizungumza leo Jumatano baada ya
kipindi cha maswali na majibu Spika Ndugai amesema anaweza kulichambua
Bunge kwa sababu alikuwepo katika vipindi hivyo na Anne Makinda na
marehemu Samwel Sitta ni walimu wake.
“Hawa ni watu nawaheshimu sana na
wamenilea sana na ni sehemu nilipofika hapa leo. Utanilinganishaje mimi
na milima mikubwa kama Kilimanjaro? Hata siku moja sikio haliwezi
kuzidi sikio,” alisema Ndugai.
Amesema katika Bunge la 9 Zitto aliwahi
kupeleka hoja ya Mgodi wa Buzwagi ambayo ilikataliwa na Bunge lakini
ikazuka hoja ya kimaadili ambapo alihukumiwa hapo hapo.
“Alihukumiwa hapo hapo akapigwa miezi
mitatu. Mnataka niende mkuku mkuku kama lile la Bunge la tisa nifanane
na mzee Sitta? Hilo pia naliweza kwa nini mnaalika matatizo nashangaa
unapambana na Spika,” amesema.
“Ninauwezo wa kupiga marufuku
kuzungumza hadi miaka yote mitano iishe hauna pa kwenda, hakuna cha
swali, nyongeza wala kuzungumza utanifanya nini?
Amemtaka kupambana na mtu mwingine lakini sio yeye.
“Kwa haya ya Spika sina sababu nayo
lakini ya kulidharau Bunge hayo sitaweza kuyavumilia nitalinda mihimili
huu kwa nguvu zangu zote,” amesema.
Amesema hawawezi kuacha wabunge
kulidhalilisha Bunge na kuhoji kwamba watachukuliaje Watanzania wengine
watakapolidhalilisha Bunge.
Amesema hilo kosa la pili kwa Zitto na kuagiza liende katika kamati ya maadili.
“Tutaenda sambamba mguu kwa mguu hadi kieleweke,” amesema.
0 comments:
Post a Comment