Klabu ya Simba leo imetangaza majina ya wajumbe watano watakaosimamia mchakato wa uuzaji hisa za klabu hiyo.
Wanachama wa Simba katika mkutano wao mkuu uliofanyika mwezi uliopita walikubaliana kubadili mfumo wa uendeshaji wake.
Wajumbe hao watano wataongozwa na jaji mstaafu Thomas Mihayo, Wakili Damas Ndumbaro, Mbunge wa Ilala, Musa Azzan 'Zungu', Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, Abdulrazack Badru pamoja na mtaalamu wa manunuzi, Yusuph Majid.
Afisa habari wa Simba, Haji Manara alisema kamati hiyo itakuwa huru na kazi yake itafanyika kwa kuzingatia weledi.
"Uuzwaji huo utafanyika kwa kuzingatia sheria za nchi. Tuna imani kubwa na timu hii tuliyoiunda kwa sababu ina watu wabobezi," alisema Manara.
0 comments:
Post a Comment