Sunday, 3 September 2017

HAYA NDIYO MANENO WALIYOAMBIWA WACHEZAJI WA ARSENAL


Wachezaji wa Arsenal wametakiwa kuacha kuishi kama watoto na kuacha kulialia.

Ushauri huo umetolewa na kiungo wa zamani wa timu hiyo, Emmanuel Petit raia wa Ufaransa.

Arsenal ambayo inanolewa na Kocha Arsene Wenger imekuwa katika wakati mgumu hasa baada ya kupoteza michezo miwili kati ya mitatu ya mwanzoni katika Premier League msimu huu.

Petit ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia 1998 amesema haya: “Ninapowaona wanacheza, wanacheza bila kuwa na moyo wa upambanaji. Lawama zinapelekwa kwa Arsene, lakini siyo kama lawama zote zinatakiwa kuelekezwa kwake.
Petit enzi akiwa Arsenal.

“Baadhi ya wachezaji hawaoni umuhimu wa kuivaa jezi ya Arsenal, na kutotambua kuwa hiyo ni moja ya klabu kubwa duniani.

“Wapata fedha nyingi kuichezea Arsenal. Ajabu ni wachache wanaoonekana kuwa na furaha, mtu anatakiwa kuwaambia kuwa hawatakiwi kuwa kama watoto kulialia. Wanatakiwa kujivunia kuivaa jezi ya Arsenal."

Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive